Sloti ya Money 5 | Ulimwengu mpya wa burudani!

0
16
Money 5 - kasino mtandaoni - online casino slots - Fazi casino games online
Money 5

Tunakuletea mchezo wa kasino wa kipekee ambapo utapata ziara ya benki. Kwa kweli, utakuwa na fursa ya kutazama ndani ya hazina ya benki. Kwa bahati ndogo tu, unaweza kujikusanyia maokoto kibao.

Money 5 ni mchezo wa sloti mtandaoni ulioandaliwa na wataalamu wa kuunda michezo ya tofauti ya kasino – Fazi. Mchezo una bonasi zenye nguvu, scatter mbili zenye nguvu, majokeri ambayo huenea katika nguzo, jackpoti na bonasi ya nasibu.

Sloti ya Money 5 - online casino slots - Fazi slots online
Sloti ya Money 5

Pata kuufahamu mchezo huu na jinsi unavyolipa pesa mtandaoni kwa kusoma mapitio ya sloti ya money 5.

Mapitio ya mchezo huu wa kasino yamegawanywa katika sehemu zifuatazo:

  • Sifa za msingi
  • Alama za sloti ya Money 5
  • Michezo ya bonasi
  • Grafiki na sauti

Sifa za msingi

Money 5 ni sloti ya kasino ambayo yenye nguzo tano zilizopangwa katika mistari mitatu na ina mistari mitano ya malipo. Ili kupata ushindi wowote, unahitaji kupata alama tatu au zaidi zinazofanana kwenye mstari wa malipo.

Hazina ya dhahabu ni alama ya pekee inayokinzana na sheria hii na inakuletea malipo hata na alama mbili katika safu ya ushindi. Michanganyiko yote ya ushindi inahesabiwa kutoka kushoto kwenda kulia kuanzia nguzo ya kwanza kushoto.

Ushindi mmoja unalipwa kwa kila mstari wa malipo. Ikiwa una mchanganyiko wa ushindi kadhaa kwenye mstari mmoja wa malipo, utalipwa ushindi wenye thamani kubwa zaidi.

Inawezekana kuunganisha ushindi wakati unawakutanisha kwenye mistari kadhaa ya malipo kwa wakati mmoja.

Ndani ya eneo la kuweka dau , kuna vifungo vya jumlisha na kutoa, ambavyo unaweza kuweka thamani ya dau kwa mstari wa malipo. Utaweza kuona thamani ya dau kwa mzunguko katika eneo la Dau .

Pia kuna fursa ya kucheza moja kwa moja , ambayo unaweza kuiamsha wakati wowote unapotaka. Kupitia chaguo hili unaweza kuweka idadi ya mizunguko isiyo na kikomo. Pia unaweza kuanzisha mchezo wa haraka.

Aidha unaweza kurekebisha kiwango cha sauti kwenye kona ya kushoto chini ya nguzo.

Alama za sloti ya Money 5

Linapokuja suala la alama za mchezo huu kama michezo mingine ya kasino, malipo ya chini zaidi ni alama za karata za kawaida: J, Q, K na A. Tano kati yao kwenye mstari wa malipo hulipa mara x20 zaidi ya dau lako.

Ikifuatiwa na alama ya noti za dola, ambazo huleta nguvu ya malipo kiasi. Ikiwa unaunganisha alama tano za aina hii kwenye mchanganyiko wa ushindi, utapata mara x40 zaidi ya dau lako.

Vibunda vya noti na matofali ya dhahabu ndio alama zifuatazo, alama hizi huleta malipo yanayofanana. Ikiwa utaunganisha alama tano za aina hii kwenye mchanganyiko wa ushindi, utapata mara x100 ya dau lako.

Alama ya msingi zaidi ya sloti hii tofauti na michezo mingine ya sloti ni hazina ya dhahabu. Alama hii inawakilishwa na mlango wa hazina. Ikiwa unaunganisha alama tano za aina hii kwenye mchanganyiko wa ushindi, utapata mara x600 ya dau lako. Huu ndio wakati wako wa kupata ushindi mkubwa.

Michezo ya bonasi

Alama ya Jokeri inawakilishwa na mrembo, mwanamke mweupe katika gauni jekundu. Inachukua nafasi ya alama zote, isipokuwa alama ya scatter, na husaidia kuunda mchanganyiko wa ushindi.

Sloti ya Money 5 - online casino slots - kasino mtandaoni - Fazi
Alama ya Jokeri

Inaonekana kwenye nguzo ya pili, ya tatu na ya nne tu. Kila wakati inapoonekana kwenye nguzo kama alama pori(wild) itapanuka na kusambaa kwenye nguzo nzima.

Mchezo huu wa sloti una scatter mbili na zote zinawakilishwa na sarafu za dhahabu. Sarafu ya dhahabu yenye nembo ya dola ya kijani ni scatter ya kwanza na inaonekana kwenye nguzo ya kwanza, ya tatu na ya tano. Mara tatu za alama hizi zinaonekana kwa wakati mmoja kwenye nguzo utapata mara x20 ya dau lako.

Scatter ya pili inawakilishwa na sarafu ya dhahabu yenye nembo ya dola nyekundu na inaonekana kwenye nguzo zote. Inaleta malipo popote inapoonekana kwenye nguzo kwa idadi ya kutosha. Scatter tano kwenye nguzo hulipa mara x100 ya dau lako.

Sloti ya Money 5 - Online casino slots - Fazi
Scatter

Mchezo pia una bonasi ya nasibu ambayo inaweza kukuongezea ushindi. Unahitaji kukisia rangi ya karata inayofuata inapovutwa kutoka kwenye kibunda cha karata.

Sloti ya Money 5 - Online casino slots - Fazi
Bonasi ya nasibu

Pia kuna jackpoti tatu endelevu ambazo unaweza kushinda kwa nasibu. Hizi ni jackpoti za dhahabu, jackpoti za platinamu na jackpoti za almasi.

Grafiki na sauti

Mazingira ya sloti ya money 5 yamewekwa katika benki, au kwenye hazina ya benki. Sauti zisizo na kero za jazz zitakuburudisha wakati wote ukiwa unacheza.

Grafiki za sloti hii ni kamilifu na alama zimeonyeshwa kwa undani.

Usikose bonge la shangwe, cheza Money 5, ulimwengu mpya wa burudani!

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here