Nicer Dice 40, an online slots game

Nicer Dice 40 | Uhondo wa kete upo hapa!

Tumekuletea burudani nyingine ya kusisimua, ni mchezo wa sloti ambao utafurahia matunda yake matamu. Hata hivyo, matunda hayo si kivutio pekee, kwani kuna mengine makubwa yanakungoja, kaa chonjo ujionee hatua kwa hatua.

Nicer Dice 40 ni sloti ya mtandaoni iliyowasilishwa na mtoa huduma Amatic Online. Mambo makubwa yanakusubiri katika mchezo huu. Takribani alama zote zimepangwa kwa mtiririko (stacked), na kuna alama za wild pamoja na wild zenye vizidishi (multipliers).

Nicer Dice 40
Sloti ya Nicer Dice 40

Iwapo ungependa kujua zaidi kuhusu mchezo huu, tunakushauri uendelee kusoma makala hii ambapo tunakuletea mapitio kamili ya sloti ya Nicer Dice 40.

Mapitio ya mchezo yamegawanywa katika sehemu zifuatazo:

  • Taarifa za msingi

  • Alama za sloti ya Nicer Dice 40

  • Bonasi za mchezo

  • Michoro na sauti

Taarifa za msingi

Nicer Dice 40 ni sloti ya mtindo wa kawaida (classic slot) yenye safu tano (reels) na mistari minne (rows), ikiwa na jumla ya mistari 40 ya kudumu ya ushindi (fixed paylines). Ili kupata ushindi wowote, ni lazima uunganishe alama tatu au zaidi zinazofanana kwenye payline.

Mchanganyiko wote wa ushindi huhesabiwa kuanzia kushoto kwenda kulia, kuanzia safu ya kwanza upande wa kushoto.

Ushindi mmoja hulipwa kwa kila payline. Endapo kuna mchanganyiko zaidi ya mmoja wa ushindi kwenye payline moja, utalipwa ushindi wenye thamani ya juu zaidi. Jumla ya ushindi huwezekana unapopata ushindi kwenye paylines nyingi kwa wakati mmoja.

Karibu na kitufe cha Spin kuna sehemu za Bet Plus na Bet Minus, ambazo hukuwezesha kuweka thamani ya dau kwa kila mzunguko.

Pia kuna kipengele cha Autoplay ambacho unaweza kukiwasha wakati wowote. Kupitia chaguo hili, unaweza kuweka hadi spins(mizunguk0) 500, pamoja na kuweka kikomo cha hasara utakachoruhusu.

Wachezaji wa dau kubwa (High Rollers) watakipenda sana kitufe cha Max Bet. Ukibonyeza kitufe hiki, dau la juu kabisa kwa kila mzunguko huwekwa moja kwa moja.

Iwapo unapendelea uchezaji wa kasi zaidi, hilo pia limezingatiwa. Unaweza kuwasha Fast Spins kwa kubonyeza kitufe chenye alama ya radi kwenye mipangilio ya mchezo. Marekebisho ya sauti yanaweza kufanywa upande wa kulia karibu na settings za sloti.

Alama za sloti ya Nicer Dice 40

Kama ilivyo kwa sloti nyingi za kawaida, alama inayolipa kidogo zaidi hapa ni cherry. Ukiunganisha alama tano za aina hii kwenye mchanganyiko wa ushindi, utashinda mara 1.25 ya dau lako.

Baada yake kuna matunda mawili ya maeneo ya joto ambayo hulipa zaidi kwa kiasi kikubwa: chungwa na limau. Yakijitokeza mara tano kwenye payline, yatakulipa mara 2.5 ya dau lako.

Sloti ya Nicer Dice 40
Alama ya chungwa

Kisha kuna jozi nyingine ya matunda inayotoa malipo makubwa zaidi, ambayo yanajulikana sana katika maeneo yetu: plamu na zabibu. Yoyote kati ya haya yakionekana mara tano kwenye payline, utashinda mara 7.5 ya dau lako.

Tunda tamu zaidi, tikiti maji, hutoa malipo makubwa zaidi miongoni mwa alama za msingi. Likijitokeza mara tano zilizounganishwa kwenye payline, utashinda mara 10 ya dau lako.

Bonasi za Mchezo

Joker(Wild) katika mchezo huu anawakilishwa na alama nyekundu za bahati. Hubadilisha alama zote na kusaidia kuunda mchanganyiko wa ushindi.

Ushindi ulioambatana na alama ya Joker/Wild kwenye mchezo wa "Nicer Dice 40".
Joker

Wakati huo huo, alama ya wild ndiyo alama yenye nguvu kubwa zaidi ya malipo. Wild tano kwenye payline zitakulipa mara 25 ya dau lako. Joker hujitokeza kama alama iliyopangwa kwa mtiririko (stacked), hivyo inaweza kujaza nafasi zote kwenye safu. Katika hali hii, unaweza kushinda hadi mara 1,000 ya dau lako.

Hata hivyo, si joker pekee kwenye mchezo huu, kwani pia kuna super joker yenye vizidishi (multipliers). Huonekana pekee kwenye safu ya tatu na inawakilishwa na kete mbili (dice).

Ushindi mnono kwenye sloti ya Nicer Dice 40.
Super Joker yenye kizidishio(multiplier)

Kila mara kete zinapojitokeza, huzungushwa na jumla ya namba zitakazopatikana ndiyo huwa kizidishi (multiplier). Kizidishi kinaweza kuwa kuanzia x2 hadi x12.

Michoro na sauti

Mandhari ya sloti ya Nicer Dice 40 yamewekwa kwenye usuli mwekundu wenye nyota zilizotapakaa. Michoro ya mchezo ni ya kiwango cha juu, huku alama zote zikionyeshwa kwa umakini wa hali ya juu.

Muziki wa sloti ni wa kawaida, lakini sauti ya ushindi huwa bora zaidi unaposhinda. Jiachilie na burudani ya kiwango cha lami kwa kucheza sloti ya Nicer Dice 40.

Post navigation

Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *