Kasino: Mambo ya Msingi Unayopaswa Kuyajua

8
1758
Bonasi ya Paris, Bonasi ya Kasino ya Mtandaoni

Kasino: Mambo ya Msingi Unayopaswa Kuyajua

Kasino ya mtandaoni ni moja kati ya starehe kubwa kwa baadhi ya watu, huku ikiwa chanzo cha mapato kwa wengine wengi. Tangu kasino ya kwanza ya mtandaoni ilipotambulishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1996 mpaka hivi leo kuna maelfu ya kasino za aina hiyo na mpaka sasa zinazidi kuongezeka.

Wingi wa kasino za mtandaoni ni kikwazo kwa wachezaji ambao wanataka kuchagua ipi waitumie, lakini sisi tunafikiri kwamba hilo ni swali la pili kwa mtu kujiuliza. Kwanza anatakiwa kuyajua haya yafuatayo kuhusu kasino ya mtandaoni ili kujiepusha na mambo mengi ikiwemo kutapeliwa na kupoteza hela nyingi bila kujua:

Fahamu sheria za kasino ya mtandaoni

Kitu cha kwanza na cha muhimu zaidi kukijua kuhusu sheria za kasino ya mtandaoni ni kwamba sheria na kanuni hizo hutofatiana kulingana na eneo analopatikana mchezaji husika. Unaweza kupita mtandaoni ukakuta orodha ya sheria za kasino ya mtandaoni, sio uamuzi mzuri kuzipitia na kuzizingatia hizo tu! Muhimu ujue kuwa mwandishi wa sheria hizo mtandaoni alilenga hadhira ambayo inaweza kuwa sio wewe!

Mwandishi anaweza kuchapisha mtandaoni sheria za kasino ya mtandaoni kuwalenga wachezaji wa nchi A lakini sheria hizo zikawa tofauti kwa wachezaji wa nchi C. 

  1. Sio kweli kwamba kila kasino ya mtandaoni hupanga matokeo ya mchezo.

Inawezekana umesikia mara nyingi kutoka kwa watu wako wa karibu, au wanachama wenzako katika makundi ya WhatsApp uvumi kwamba ‘kasino za mtandaoni’ hutumia program fulani za kompyuta kupanga matokeo na hivyo sio rahisi kushinda katika michezo hiyo. 

Ukweli kuhusu uvumi huu ni kwamba, sio kasino zote za mtandaoni zimetengenezwa kwa namna ambayo mwisho wa siku zitamfanya mchezaji asiweze kushinda. Zipo kasino nyingi za mtandaoni ambazo ni salama na zina uwanja sawa wa kushinda au kushindwa! Kwa hapa Tanzania kuna kasino za mtandaoni ambazo  ni salama kwa pesa na muda wako. Tovuti za kamari za www.meridianbet.co.tz na www.pmbet.co.tz zinasifika kwa kuwa na kasino za mtandaoni yenye uwanja sawa wa kushinda bila matokeo ya kupagwa.

  1. Baadhi ya Tovuti za Kamari Mtandaoni Husumbua Wachezaji Kutoa Pesa Zao

Imekua kawaida sana siku hizi kukuta tovuti ya kuchezesha kamari mtandaoni ikilalamikiwa na wachezaji juu ya ugumu unaowekwa na tovuti hiyo kuhusu ucheleweshwaji wa malipo ya ushindi wa kasino ya mtandaoni. Malalamiko hayo sio ya kupuuzwa, yazingatie!

Kuendesha kampuni au tovuti ya kamari mtandaoni ni biashara kama zilivyo biashara nyinginezo, waendeshaji wengi wa tovuti hizo hulenga kupata faida. Hakuna hata mmoja anaetoa huduma hii kama huduma nyingine za kijamii! Hili sio la kushangaa, ila ni vizuri faida ipatikane kwa njia halali. Tovuti nyingi zinasumbua wateja wao kupata hela zao zinalenga kuwafanya wachezaji washindwe kutoa pesa zao hivyo wapate tamaa kuendelea kuzichezea na mwishowe wazipoteze!

Ni rahisi kuona malalamiko ya wakamaria kuhusu kucheleweshewa pesa zao za ushindi na tovuti fulani ya kamari kwenye mitandao ya kujamii, ukiona hili chunguza zaidi kisha amua kama ni sahihi au sio kuamua kutumia tovuti husika. 

  1. Usihadaike na Bonasi za Ukaribisho Zinazotolewa na Baadhi ya Tovuti

Bonasi za ukaribisho kwa wateja wapya wa kasino ni moja kati ya vitu vinavyowavutia wachezaji wengi kutumia tovuti fulani, sio vibaya kuzingatia hilo. Lakini mchezaji hatakiwi kuangalia tu ukubwa wa bonasi kisha kuamua kutumia tovuti husika. 

Unaweza kukutana na tovuti inayodai kuwa inatoa bonasi ya 100% kwa wachezaji wapya watakaoweka kiasi fulani kwa mara ya kwanza.

Unaweka kiasi hicho na unapata bonasi ya 100% kweli. Yani unaweka shilingi 10,000 na unapata 10,000 nyingine bure! Ni nzuri eeh?

Ni jambo zuri mpaka pale utakapokuja kuangalia masharti yanayoambatana na bonasi hiyo. Baadhi ya tovuti huweka masharti magumu mno kuyatekeleza ili uweze kutoa hela iliyopatikana kutumia bonasi hiyo au yasiyotekelezeka kabisa. Kwa mfano, unaweza kukuta kasino inamtaka mchezaji kuizungusha bonasi aliyopata mara 50 ili aweze kuitoa! Tena pengine mizunguko hiyo inahesabika kwenye kwenye mchezo fulani iwe keno au sloti fulani tu na ukiizungusha kwenye mchezo mwingine haihesabiki!

Kwa mazingira kama hayo ni vigumu japo kuna baadhi ya wachezaji wanaweza kupatia na kushinda bonasi hizo pamoja na hayo masharti. 

  1. Kamari Huleta Uraibu

Kama unafikiri hauwezi kupata uraibu wa kamari eti kwa sababu kamari sio kinywaji au chakula kinachoingizwa mdomoni, UNAKOSEA! 

Binafsi nimekutana nakuongea na watu wengi waliokumbwa na uraibu wa kamari iwe za mtandaoni au kwenye vibanda, iwe kwenye kasino au ubashiri wa michezo! 

Nimekutana na watu wengi waliofikia hatua za kupoteza pesa nyingi kwenye kamari, wengine walifikia hatua ya kuuza vitu vyote wanavyomiliki na pesa yote ikapotelea kwenye kamari! Wengine wakaingia kwenye madeni mengi na yasiyolipika kisa kamari hususani kasino ya mtandaoni! 

Unashauriwa kuzingatia ku ‘BET RESPONSIBLY’. Jifanyie uchunguzi kidogo uone kama pesa unayoitumia kwenye kamari huwa inaathiri mambo yako mengine ya muhimu ama la, kama ndivyo jua unauelekea uraibu wa kamari. Pata msaada haraka kabla mambo hayajakuharibikia zaidi.

Michezo yote ya kamari, ziwe za mtandaoni ama la, za kasino au sports betting ni vema zifanywe kama burudani tu na sio chanzo cha mapato.

Hitimisho

Tunaweza kuandika mengi kuhusu kasino ya mtandaoni ili yawafae wakamaria wapya kwa wazoefu, lakini ukweli ni kwamba hatuwezi kuandika yote kwa wakati mmoja. Hii ni pengine kwa sababu kasino ya mtandaoni ni mchezo mpya kwa wakamaria wengi hivyo wana mengi ya kujifunza.

Hivyo basi makala hii inaweza kuwa msaada mkubwa na imejibu baadhi ya maswali ya wakamaria wengi, hivyo basi unaombwa kukumbuka kitembelea tovuti hii kila siku ili uweze kujifunza nasi zaidi.

8 COMMENTS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here