Bonasi ya Kasino Mtandaoni

Kasino ya mtandaoni imezidi kujizolea umaarufu siku za hivi karibuni kuliko kasino ya kawaida. Sababu kubwa ya umaarufu wa kasino ya mtandaoni ni bonasi zinazotolewa na wamiliki wa kasino hiyo. 

Waandaaji wa kasino hizo hutoa bonasi na promosheni ambazo mara nyingi hutofautiana na waandaaji wengine, hivyo basi ni vema kwa wachezaji kujua vigezo na masharti vya bonasi husika kabla ya kuitumia.

Aina za Bonasi ya Kasino Mtandaoni

Kunaweza kuwa na aina mbalimbali za bonasi za kasino kutegemeana na matakwa ya mchezaji na kampuni husika, lakini aina kuu ni za bonasi hizi ni mbili: Aina ya kwanza ni bonasi zile ambazo mteja ili azipate inamlazimu kuweka kiasi fulani cha pesa katika akaunti yake, na aina nyingine ni zile ambazo mchezaji anapata bila kuweka kiasi chochote cha pesa. 

Ili kupata bonasi ya baada ya kuweka pesa, mchezaji anatakiwa kwanza kujisajili au kufungua akaunti katika tovuti ya kampuni husika na kisha weka kiasi cha pesa kwenye akaunti hiyo kama ambavyo vigezo na masharti ya kampuni husika vinataja. Kila kasino ina kiasi chake ambacho inamtaka mteja kuweka ili kupata bonasi hiyo. 

Kwa upande wa bonasi zisizolazimisha mchezaji kuweka kiasi chochote cha pesa ili azipate, mambo ni rahisi tu kwani atatakiwa kujisajili tu kisha anapata bonasi na promosheni husika. 

Promosheni Gani Hutolewa Kwenye Bonasi Hizo?

Hizi ni baadhi ya promosheni ambazo mchezaji anaweza kuzipata katika bonasi ziwe za baada ya kuweka fedha katika akaunti ya mchezaji au za bila kuweka fedha yoyote katika akaunti. 

  • Bonasi 100% ya Kiasi cha Kwanza Kuwekwa

Promosheni hii inaangukia katika kundi la bonasi za baada ya kuweka pesa katika akaunti ya kasino ya mtandaoni ya mteja. Kupitia bonasi hii mteja wa kasino anapata nyongeza ya pesa sawa na kiwango alichoweka kwa mara ya kwanza, yani 100%. 

Mara nyingine bonasi hii inaweza kuwa ndogo kufikia asilimia 60 ya kiwango kilichowekwa kwa mara ya kwanza, au kuwa kubwa zaidi mpaka kufikia mara nne ya kiwango husika.

  • Mizunguko ya Bure kwa Michezo Fulani

Mara nyingi promosheni hii huwa sehemu ya bonasi zinazotolewa bila ya mchezaji kuweka pesa yoyote katika akaunti yake. Baada ya kujisajili na kasino ya mtandaoni, mchezaji hupewa mizunguko kadhaa ya bure kutakiwa kuwa ameitumia na kuimaliza katika sloti husika kabla ya muda fulani kupita. 

Watu wengi hawapendelei mzinguko hii ya bure kwani haimpi mchezaji uhuru wa kuchagua sloti ya kuitumia na badala yake atatakiwa kuitumia katika sloti iliyoamriwa tu! Kama haipendi au kuiweza anakuwa amepoteza mizunguko hiyo. 

Masharti ya Matumizi ya Bonasi za Kasino Mtandaoni 

Mara zote kila bonasi na promosheni ya kasino mtandaoni huja na masharti na vigezo vya namna ya kuitumia ili kuzuia udanganyifu miongoni mwa wateja wao. Wamiliki wa kasino hizo mtandaoni huwa wanaweka masharti ya matumizi ya bonasi husika ili kuzuia wateja wenye lengo la kujisajili tu ili wapate pesa ambazo hutolewa kama bonasi na kisha kuzitoa. 

  • Sharti kubwa na la kawaida kwa makampuni mengi juu ya matumizi ya pesa ya bonasi ni kwamba huwa yanataka pesa ya bonasi izungushwe mara kadhaa katika michezo ya kasino kabla haijatolewa.

Idadi ya mizunguko inaweza kuwa yoyote kati ya miwili hadi sitini! Yani pesa utakayoshinda kutumia bonasi lazima uichezeshe tena kwa idadi hizo ulizoelekezwa na masharti ya bonasi husika. 

Hili linaweza kuwa gumu kidogo na gum huo unaongezeka kila idadi ya mizunguko inapokua mingi zaidi kwani ukweli ni kwamba unapozidi kuitumia bonasi ya kasino mtandaoni mara nyingi zaidi ndivyo unavyojiweka katika hatari ya kuipoteza. Hivyo basi mchezaji anashauriwa kuchagua bonasi yenye masharti ya mizunguko michache. 

  • Sio kila sloti inahesabika katika mahesabu ya mizunguko husika.

Ni kawaida kukuta kasino imemewekwa sharti kwamba michezo yote ya kasino  itahesabiwa katika idadi za mizunguko inayokamilisha sharti la mizunguko 20×, 30× au idadi nyingine yoyote iliyowekwa ili mchezaji akidhi kutoa pesa aliyoipata kama bonasi ya kasino mtandaoni.  

Ni vizuri mchezaji akasoma vizuri masharti ya bonasi husika ili kuzuia upotevu wa muda na pesa. 

  • Muda huzingatiwa katika utoaji wa bonasi

Kasino zote za mtandaoni hutoa muda fulani wa bonasi yake kuwa hai kabla ya kuonekana imeisha muda wake wa matumizi. Muda huo unaweza kuwa wiki mbili, mwezi mmoja, miwili au kipindi chochote ambacho kimewekwa na kasino husika. Hivyo mchezaji anashauriwa kupitia kwa umakini masharti ya bonasi husika kabla hajaamua kuitumia.

Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara Kuhusu Bonasi za Kasino Mtandaoni

  • Ni salama kutumia bonasi ya kasino mtandaoni?

Jibu la swali hili lineweza kuwa ndiyo au hapana kutegemeana naazingira.

Kwa mazingira ambayo bonasi hiyo inatolewa na kasino iliyosajiliwa rasmi na inaendesha shughuli zake ikitambuliwa na mamlaka husika hususani bodi ya michezo ya kubahatisha, jibu ni NDIYO!

Hata hivyo jibu la swali hili linaweza kuwa HAPANA iwapo kasino husika inaendesha shughuli zake za kubashiri na michezo mingine bila kusajiliwa rasmi. Katika mazingira haya hata ukidhulumiwa hela uliyoipata katika bonasi hautokua na namna ya kushtaki popote. 

  • Ni Kwanini Kasino za Mtandaoni Hutoa Bonasi? 

Inaweza kuonekana na wengi kuwa kasino zinajitafutia hasara kwa kutoa pesa za bure kama bonasi. Lakini ukweli ni kwamba mwisho wa siku zinatengeneza faida nyingi mno.

Zipo bonasi ambazo hutolewa hutolewa kwa wateja wapya, hizi ni muhimu kwa kasino ili kuwawezesha kuvuna wachezaji, kwa kesi hii ni ‘wateja’ wapya. 

Bonasi zingine hutolewa kwa wateja wanaofanikiwa kutumia kasino husika kwa muda fulani unaoonekana kuwa mrefu. Hizi husaidia kasino kuwafanya wateja waendelee kutumia huduma zao tena na tena kwa matumaini kuwa mwisho wa siku watapata bonasi hiyo. 

  • Ninaweza Kushinda Pesa kwa Kutumia Bonasi ya Kasino Mtandaoni? 

Ndiyo, unaweza kutengeneza pesa ya kutosha kwa kutumia bonasi. LAKINI jambo hilo sio rahisi kama ilivyo ukitumia pesa yako ya kawaida. Hii ni kutokana na ukweli kwamba bonasi huja na masharti mengi ya namna ya kuitumia ili uweze kutoa pesa itakayopatikana kama ushindi, masharti hayo yasipotimizwa bonasi na kiasi chochote kilichopatikana kama ushindi wa bonasi hiyo hakiwezi kutolewa. 

Hivyo basi:

Mchezaji anaweza kuona kuwa bonasi na promosheni za kasino ya mtandaoni hazina faida kwa sababu zinakuja na masharti mengi magumu kuyatimiza. Sisi tunaona anaweza kuwa sahihi kwa upande mmoja na asiwe sahihi kwa upande mwingine.

Ukitazama maana ya faida za bonasi ya kasino mtandaoni kwa upande wa pesa unayoweza kushinda papo kwa papo, huwezi kuona kuwa bonasi hizi zina faida. Lakini unatakiwa kufikiria hata mbali zaidi ya hapo, fikiria kwamba hata kama bonasi ya kasino mtandaoni inakuja na masharti mengi na magumu kuyatekeleza lakini ni njia nzuri kwa wewe kujipatia uzoefu na ujuzi wa sloti husika kabla hujaamua kuicheza kutumia hela yako halisi.

17 Replies to “Bonasi ya Kasino Mtandaoni”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *