

Tutakubaliana kwa hakika kwamba sisi sote ni wacheza kamari – iwe ni unapenda kucheza poka mtandaoni, unajaribu bahati yako kwenye mitandao mbalimbali katika kutabiri matokeo ya tukio fulani ama unabetia timu yako unayoipenda zaidi – hakika kila mmoja wetu ni mkamaria!
Ukishasikia hivyo sasa ni hakika kuwa tunatakiwa kuwa makini mara kwa mara tunapofurahia michezo hii na kuhakikisha kwamba kubashiri kwetu hakuzidi kiwango na tunacheza kwa ustaarabu mkubwa.
Leo, hapa onlinecasinobonus.co.tz tumekuja na undani kidogo wa kuhusu kubeti kusiko kistaarabu na ambako kumepitiliza sana. Twende sawa sasa…
Nini maana ya kubeti kusikofuata ustaarabu?
Kuna aina tofauti za kubashiri ambako hakuzuiwi na uwepo wa mashine za sloti za mitandaoni, karata, kasino za hewani au kubetia michezo ya kawaida, na zote hizo zinaweza kufanya mtu akabashiri isivyo kistaarabu na kuzidi kiwango.
Hii inaweza kutokea kwa yeyote yule bila kujalisha aina ya mtu, umri, jinsia, asili yake, kazi yake ama elimu yake.
Kwa tafsri za haraka, kubashiri bila ustaarabu ni kitendo cha kubashiri kwa kupitiliza na kushindwa kujizuia kabisa. Inaweza kuwa na matokeo mabaya kwa wapendwa na watu wa karibu wa mteja husika.
Haijalishi hali ikoje – iwe mteja yuko sawa ama hayuko sawa kiakili, akiwa na pesa ama asiwe nazo – yeye ataendelea tu kubashiri bila ya kujali madhara yake kwa namna mbalimbali. Hata kama mteja hawezi kukubali kushindwa, ataendelea kubashiri akihatarisha hali yake na hivyo kupatwa na hisia kali na kuamua kubashiri kwa hasira na hivyo kujihatarisha zaidi.
Tofauti ya kubashiri kulikopitiliza na matatizo ya kubashiri
Kushindwa kujizuia kubashiri kwa kiwango kikubwa na kuzidiwa na matendo ya kubashiri – yote haya yanafanana sana lakini maana zake ni tofauti kabisa.
Hayo yote ni yale ambayo yatapelekea uwe na hatari ya kuharibiwa kimaisha endapo usipokuwa makini nayo. Utapoteza muda mwingi pamoja na pesa nyingi.
Hii yote ni ile ambayo inahusisha kubashiri kunakohatarisha maisha yako. Akili inakuwa inawaza kupata zaidi na zaidi na kutotosheka na ulichopata au ulichopoteza na kuzidi kujaribu kwa muhemko na hasira.
Sababu za kushindwa kujizuia
Inaweza kuwa inasababishwa na suala la kibaiolojia kwamba unahitaji pumziko na faraja na kuhisi kwamba sehemu sahihi ni kwenye kubashiri.
Ama inaweza kuwa ni masuala ya kiuchumi na kuamini kwamba unaweza kulala maskini na kuamka tajiri ndani ya siku moja pekee. Ama kuendelea kufukuzia pesa iliyopotea kwa hasira na muhemko.
Kukosekana kwa imani ya kidini nako ni sababu mojawapo ya kubashiri kwa kupitiliza na pasipo kujizuia kabisa.
Dalili za kushindwa kujizuia kubashiri
Tatizo hili linaweza kuwa ni la kila mmoja wetu bila kujali hali zetu. Inapotokea kwa mtu wako wa karibu ama wewe mwenyewe basi ni hakika kuwa itakuwa ikikuumiza na kukusumbua akili yako. Ukivuka mstari wa ukomo utajikuta unaanza kujenga mazoea mabaya na tabia hatarishi sana katika jambo hili na pengine kuharibu zaidi miendeno yako kwa ujumla.
Endapo umekuwa ukijuliza mtu aliyeathiriwa na kubashiri anakuwaje basi leo utafahamu zaidi na unapaswa kuzingatia haya kwa undani kabisa:
- Je, umekuwa ukijishtukia namna unavyoshiriki kubashiri?
- Tabia yako ya kubashiri inashindwa kuzuilika kabisa?
- Umewahi kukopa ili ukabashiri?
- Unafukuzia mapato uliyoliwa katika kubashiri na kutaka kuyarudisha?
- Je, familia yako ama marafiki zako wanahofia tabia zako na kukuhofia wewe mwenyewe?
Endapo ukiona haya yote yanakuhusu ama mengi kati yake yanakuhusu basi ni muda muafaka wa wewe kutafuta suluhu yake mapema kabisa.
Unawezaje kujizuia kubashiri kulikopitiliza?
Kwa kweli hakuna kitu kigumu kama kuacha kushiriki katika michezo hii na kukubali kwamba umepitiliza kiwango kwa kiasi kikubwa sana.
Hata kama ukifika hatua ya kujiuliza ni namna gani unaweza kujitoa katika tatizo hilo basi ujue unaweza kusaidika na kuachana na tabia hatarishi zinazojitokeza ili uweze kubashiri kistaarabu kabisa.
Lengo ni kurudi kwenye mstari wako wa mwanzo na kubashiri kistaarabu bila ya kujisababishia matatizo wewe mwenyewe ama kwa wapendwa wako, zingatia haya:
- Amua kubadilika
- Jifunze namna ya kutatua matatizo kwa njia nzuri zaidi
- Wasiliana na marafiki na uzungumze na ndugu
- Geukia mashirika yanayosisitiza kubashiri kistaarabu kwa msaada zaidi
- Jiunge na makundi ya msaada katika sekta hii
- Tafuta kitu mbadala kama vile kucheza mpira, kuogelea ama kusikiliza muziki
- Pangilia vyema muda wako wa kufanya mambo
Kwa hiyo, endapo unajihisi kuwa unapotea na kushindwa kabisa kujizuia hebu jitahidi kuepuka kukaa peke yako ukiwa na kompyuta yako ama simu na kuepuka aina zote za ushawishi unaoweza kujitokeza.
Kumbuka kwamba kila tatizo lina suluhu yake na pia hili nalo lina suluhu! Tafadhali fikiria kuhusu kujitoa katika kubashiri kulikopitiliza na kupumzika kidogo kwa muda kabla hujaendelea.
Endapo unawaza juu ya tiba ya kutoweza kujizuia kubashiri hizi hapa ni aina za ushauri unaoweza kuutumia:
- Anza tiba mapema
- Hudhuria klabu za kuzuia kufanya mambo kwa kiwango kilichopitiliza
- Jiunge na mijadala ya kujizuia kufanya mambo yanayohatarisha hali yako
- Hudhuria semina na vituo vya ushauri nasaha wa masuala yanayohusiana na haya
Kwa kumalizia…
Hapo juu tumeshaeleza namna nzuri ya kujua dalili za mtu aliyeshindwa kujizuia kabisa kubashiri kwa kiwango cha wastani na hivyo ni muhimu sana mtu akafahamu muda wa kuhitaji msaada zaidi pale anapokwama yeye binafsi au kutoka kwa ndugu na marafiki zake.
Ukiona haya yafuatayo ujue kabisa unahitaji msaada zaidi:
- Unaficha ficha mambo yako ya kuhusiana na kubashiri
- Unapata wakati mgumu kujizuia kubashiri pamoja na tabia za kubashiri
- Kukopa pesa ili ukabashiri
- Kusikia watu wakikuongelea kuwa wewe umepitiliza katika kiwango kizuri cha kubashiri
Kumbuka kwamba kubashiri kistaarabu ndiyo mpango mzima! Kubashiri kistaarabu ni kitu kigumu lakini kinawezekana na inahitaji umakini tu.
Asante sana kwa elimu nzuri juu ya ubashiri
Kwa kweli somo la kubeti kistaarabu inabidi mrudie mrudie ili tupate elimu.tusibeti kupitiliza
Nimembenda sana sheria zenu
Asanteen Sana kwaerimu nzuri yakujua kubashili
Ushauri mwanana kwa wakamaria. Ni vema kila mmoja wetu akajua hili#meridianbettz
Ushauri mzuri sana wengi hatujui mambo haya asanten meridianbet kwa kutujuza
Huu mchezo unatakiwa kucheza kiasi na kistaarabu
Great games thanks #meridianbet
Game slot nzur sana hii 👍
Kubashiri kistaarabu ndi vizuri asante kwa kutukumbusha #meridianbettz
Ushauri mzuri sana.asanten
hata ufanyeje kamari ni kamari hauwez ukaniambia kuwa mchezo wa kamali ni mchezo wa kisrabu nikishaliwa hata nauli hamnipi jalibuni kiangalia hapo nakuja na hela zangu hadi ya kodi namalizia hapo bac mkinila mnipe nauli akuna nyie watu#meridianbettz
Kubet kwa kutumia simu ya mkononi bila kujuwa mtu mwingine
N furaha kuwa kupata maelezo jinsi ya kubashiri maana tulikuwa tunabashiri bila kujua nini maana ya kubeti na kamari hivyo asante online casino kwa maalezo hayo
Ila mnachelewa kuapprove pesa ukishinda fanyeni maboresho
Aisee mmenifundisha jambo moja zuri sana Meridian
Kumbe n rahisi kiasi hicho habari njema kutoka online casino tz
Huu mchezo upo vizuri na waumakini Sana Melidian mnatuweza sisi wateja
Safi Sana kwa ushauri mkwanja kimya kimya na kisimu chako
Comment*meridianbet ndiyo betting pekee inayokidhi mahitaji yetu wateja wao, asante sana kwa ubunifu wenu
Hakika kuna michezo mingi sana na meridianbet casino
Kasino ya kibabe
da kwer san bet kistaarab
Game slot nzur sana hii 👍